Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, katika video kadhaa zilizosambazwa kwa wingi siku ya Jumatatu katika mitandao ya kijamii, kijana mwenye umri wa miaka 18 anaonekana akipeperusha bendera ya Palestina akiwa ndani ya basi lisilo na paa. Kijana huyo ni Lamine Yamal, supastaa wa soka wa Barcelona, ambaye alikuwa akijibu kwa tabasamu shangwe za mashabiki.
Barça ilitwaa taji lake la ishirini na tisa la La Liga baada ya kuishinda Real Madrid, mpinzani wake wa jadi, kwa mabao 2-0 siku ya Jumapili. Hii ni mara ya pili katika historia yao kutwaa ubingwa huo wa ligi kuu.
Tangu kuanza kwa mauaji ya kimbari huko Ghaza mnamo Oktoba 2023, mji wa Barcelona umekuwa moja ya vituo vikuu vya harakati za kuiunga mkono Palestina nchini Hispania.
Mahali hapo pia limekuwa kitovu cha maandamano makubwa na yenye mshikamano ya wafuasi wa Palestina, na vilevile limekuwa sehemu kuu ya kuondokea meli za misaada zilizokuwa zikijaribu kuvunja mzingiro wa Ukanda wa Ghaza uliowekwa na utawala wa Kizayuni wenye umwagaji damu.
Chanzo: TRT

Maoni yako